Search Results for: LINEX

Video Queen ‘Erycah’ Aifungukia Siku Yake Ya Kwanza Faragha…!!

WIKI hii kwenye 10 Questions tunaye video queen anayekuja kwa kasi Bongo, huyu si mwingine bali ni mwanadada anayefahamika kwa jina la Ericka Daniel Moshi ‘Erycah. Anafunguka mambo mbalimbali kupitia maswali aliyoulizwa na Mwandishi Wetu. Fuatilia hapa chini…

erycah erycah_kwa_hela_linex

Mwandishi: Habari ya mjini ni kwamba uli-date na msanii Linex baada ya kumaliza kufanya naye ile video ya Kwa Hela, una lipi la kujitetea?
Erycah: Si kweli na napenda Watanzania wajue kuwa sijawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Linex zaidi ya ule wa kikazi tu.

Mwandishi: Hivi ni kwa nini uliamua kujiingiza kwenye kazi ya ‘kuuza nyago’ na si kazi nyingine?
Erycah: Niligundua kuwa, kwa muonekano wangu ningeweza kufanya vizuri ndiyo maana nikaamua kuja huku..

Mwandishi: Kama si u-video queen unadhani ungekuwa unafanya shughuli gani kwa sasa?
Erycah: Kwa kuwa napenda sana biashara basi ningejikita kwenye ujasiriamali.

Mwandishi: Hadi kufikia hapo ulipo umeshawahi kutoka na wanaume wangapi?
Erycah: Kusema ule ukweli kabisa ni watatu tu. Nione hivihivi lakini ni msichana ninayeuthamini sana mwili wangu.

Mwandishi:Ni yupi ambaye umewahi kumpenda kati ya wote na kwamba uliumia sana mlipoachana?
Erycah: Naomba nisimtaje maana at ajisikia sana huko aliko na najua tayari ana mtu mwingine.

Mwandishi: Mara ya kwanza kabisa kukutana faragha na mpenzi wako ilikuwaje?
Erycah: Sijui hata nisemeje kwa kuwa nilipata wakati mgumu ambao hauelezeki. Sitaki hata kukumbuka siku yangu ya kwanza faragha.

Mwandishi: Kwani uliingia kwenye uhusiano wa kwanza wa kimapenzi ukiwa na umri wa miaka mingapi?
Erycah: Dah! Maswali mengine bhana! Nilikuwa na miaka 18.

Mwandishi: Nini kinakuumiza kwenye mapenzi?
Erycah: Kudanganywa kama mtoto mdogo sipendi kabisa.

Mwandishi: Wengi wanaoonekana wakiuza nyago kwenye video za wasanii wameishia la saba na wengine kidato cha nne, wewe elimu yako ikoje?
Ericka: Nimemaliza diploma ya Record Management pale Chuo cha Magogoni, kama Mungu akijalia mwakani nitaendelea.

Mwandishi: Mavideo queen wengi wanadaiwa kuitumia fani hiyo kujiuza, kwako hilo likoje?
Erycah: Unajua kila mmoja ana akili zake, mimi nafanya kazi hii kama zilivyo nyingine sasa kama wapo wanaojiuza kwa staili hiyo ni wao na maisha yao.

chanzo: GPL

KIKI ZA MASTAA ZILIZOTINGISHA, SHILOLE, VANESSA MDEE, RAY KIGOSI, RUBBY, ASLAY…!!

KIKI siyo kitu kigeni kabisa kwa wasanii ulimwenguni. Kutafuta jambo la kushtua na kuwafanya mashabiki wamzungumzie msanii husika kwa muda mrefu zaidi akiwa na lengo la kuachia kazi yake.

Lakini kwa baadhi ya wasanii wetu hapa Bongo hujiingiza kwenye skendo wakidhani ni kiki. Kwa kawaida kiki ni nzuri ili kumsaidia msanii kujipaisha na kuchomoa kazi yake, lakini si kwa kujiharibia kwa kashfa mbaya ambazo mwisho wake kufutika inakuwa shida.

Yes! Hapa Bongo wapo mastaa wengi ambao wametingisha kwa kiki huku wengine wakijaribujaribu. Hizi ni baadhi ya kiki za mastaa zilizotingisha zaidi tangu kuanza kwa mwaka huu.

RUBY, ASLAY

Kila mtu aliongea lake ilipovuma kuwa Ruby anatoka na Aslay ambaye kiumri ni mdogo kwake. Hii ilitokea Juni 13, mwaka huu mara baada ya Ruby kuanza kutupia picha za Aslay kwa fujo kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika meneno yanayoashiria kuna mahaba mazito kati yao.

kiki

Aslay yeye alimjibu Ruby kwa jumbe tamu za mahaba na kuzidi kuwachanganya mashabiki huku wengi wakitamani kuona kama penzi hilo jipya mjini litakuwa na uzito wa kuipiku kapo ya Harmonize na Wolper iliyokuwa inatamba kipindi hicho.

Wakati watu wengi wanazidi kumiminika na kuifuatilia kapo hii ndipo Yamoto Band wakaachia ngoma yao mpya inayoitwa Suu, waliyomshirikisha Ruby.

Ikasanuka kumbe ilikuwa kiki tu. Hilo lilithibitishwa hata na meneja wao Said Fella ‘Mkubwa Fella’ a.k.a Mheshimiwa Diwani.

LINEX

“Ahsante Mungu, kuna maamuzi hayahitaji matangazo, silence speaks volumes,” aliandika Linex kwenye ukurasa wake wa Instagram mara baada ya kutupia picha akiwa kwenye mikao tofauti na mrembo aliyedai kuwa amemuoa.

Linex alizidi kupokea pongezi kutoka kwa mashabiki waliovutiwa na tukio la yeye kufunga ndoa, uamuzi ambao ni nadra mno kwa wasanii wa Bongo Fleva.

Hali ilikuwa tofauti mara baada ya kutumia picha zilezile za harusi kutengeneza kava la ngoma yake mpya iitwayo Kwa Hela, aliyoachia mwanzoni mwa mwaka huu.

Kwa tukio hilo, Linex alijikuta akipokea matusi kutoka kwa mashabiki kwa kosa la kuchezea hisia zao lakini mbali na kadhia hiyo lengo lake la kutumia Kiki lilifanikiwa, aliapoachia ngoma yake ikapenya.

RAY KIGOSI

Vincent Kigosi ‘Ray’ alifanikiwa kuwakamata mashabiki wake kwa kutengeneza kiki yenye ‘akili’ sana. Yeye aliibuka na maelezo kuwa weupe wake ni kwa sababu anatumia maji mengi na kushiriki mazoezi.

Ray alisema hayo wakati akihojiwa na kituo kimoja cha runinga jijini Dar es Saalam. Hakuna kiki inayofikia hii tangu mwaka huu umeanza. Katika mitandano ya kijamii watu mbalimbali walipiga picha wakiwa wanakunywa wakidai wanataka kuwa weupe kama Ray!

Ile kushangaashangaa, Ray akaachia Filamu ya Tajiri Mfupi ambayo ilifanya vizuri sokoni. Pamoja na kiki hiyo, Tajiri Mfupi ni kati ya sinema bora za Kibongo zilizotoka mwaka huu.

VANESSA MDEE

“Nikupe Kiki ujulikane au siyo? Kila siku twanyamaza ndiyo mtugaragaze. Mimi siyo wale uliowazoea,” aliandika Vanessa Mdee kwenye instagram akimshambulia Shilole.

Shilole hakukaa kimya naye kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika: “Veepe jipange sana, mwenzio Igunga niliaga, sijaletwa kwa kubebwa kwenye lori, nimekuja na mbio za mwenge. We si wa magorofani na kiingereza chako cha kuunga mi ndo mtoto wa mbwa, sasa ole wako tukutane utanyooka.”

Watu wakahamishia mawazo yao kwao, kutahamaki kumbe walikuwa wanaandaa shoo Club Bilicanas, Dar. Shoo ilikuwa poa kutokana na kiki hiyo.

NEDY MUSIC

Baada ya Shilole kumwagana na Nuh Mziwanda watu walikuwa wanatamani kufahamu ni nani ataziba pengo hilo. Ghafla kijana mdogo Nedy Music akaanza kuhisiwa kutoka kimapenzi na mwanadada huyo.

Sababu kubwa iliyofanya watu waanze kuhisi kuwa kuna penzi kati yao ni picha walizokuwa wanatupia kwenye Instagram zikiambatana na maneno ya mapenzi.

Hakuna aliyemjua Nedy Music kabla ya kuwa na Shilole lakini alipata umaarufu mara baada ya kiki hiyo ya kumrithi Nuh Mziwanda, hata alipoachia ngoma yake Usiende Mbali chini ya Ommy Dimpoz kupitia lebo ya PKP alichomoka kirahisi tu.

Na hapo ndipo ikajulikana kuwa hakukuwa na mapenzi kati yao bali ilikuwa kiki ya kutafuta mashabiki kwenye muziki huu wenye ushindani. Kwa hilo alifanikiwa.

PHOTOS: USIKU WA NGWAIR @ MAISHA BASEMENT – PALIKUA HAPATOSHI…!!

Jana ndani ya Maisha Basement palikua hapatoshi maana moto uliwaka, ulikua ni usiku maalum wa kumkumbuka marehemu Albert Mangwear aka Ngwair. Lilidondoshwa show la kufa mtu likisindikizwa na vichwa kibao kutoka kwenye kiwanda cha Bongo Flava na hihop tanzania kama TID Mnyama, Dudubaya, Linex, Belle9, Mirror, M to The P, Jay Moe na wengine kibao.

ngwair ngwair2 ngwair3 ngwair4 ngwair5 ngwair6 ngwair7 ngwair8 ngwair9 ngwair10 ngwair11 ngwair12 ngwair13 ngwair20

PHOTOS: MREMBO HUYU NDIO USINGIZI WA ‘LINEX’…!!

Unamkumbuka yule mtoto mrembo kwenye video ya ‘Kwa Hela’ ya Linex Sunday Mjeda? Kupitia mahojiano maalum na kipindi cha E-News cha EATV linex amefunguka kuwa huyo ndiye mpenzi wake kwa sasa. Mtazame halafu tupe maoni yako kama anahusika…

linex linex2 linex3 linex4 linex5

linex6

sunday sunday2

 

LIST YA WASANII WATAOTUMBUIZA KATIKA SERENGETI FIESTA DAR 2013…!!

davido

List ya wasanii wawili kutoka nje ya Tanzania ilitangazwa, ambao ni Alaine (Jamaica) na Davido (Nigeria) ambae alithibitisha kushuka na J.Martins, sasa leo hii wasanii wawili zaidi wamethibitishwa kushuka ikiwa ni Mohombi  pamoja na Iyanya kutoka Nigeria.

Na hawa ndio wasanii wetu watakao share stage moja na wasanii hao

Ommy Dimpoz, mwana FA na AY, Rich Mavoco, Makomando, Weusi, Linah, Shilole, Snura, Recho, Young Killer, Stamina, Country Boy, Godzilla, Cassim, Quick Rocka, Juma Nature, Ney wa mitego, Madee, Nikki Mbishi, Kala Jeremiah, Linex, Chidi Benz, Shettah, H Baba, Samir, Darasa, Afande Sele, Baba Levo, Peter Msechu, Mabeste, Mirror, Menina, Walter, Nuhu, Cliff Mitindo, Blue, Young D, Dully, Amini, Christian Bella, TID, Kala Pina, Ney Lee, Fid Q, Ben Pol, Vanessa, Chege